Author Information

Maelekezo kwa Waandishi (Author Guidelines)

Wakati wa uandishi wa makala mwandishi azingatie na kufuata yafuatayo:

  • Urefu wa makala uwe baina ya maneno 3,500 hadi 7,000 yakijumuisha ikisiri na marejeo.
  • Ikisiri iwe na maneno baina ya 200 na 300 na ifuatiwe na maneno muhimu yasiozidi matano.
  • Makala iandikwe kwa lugha ya Kiswahili Sanifu.
  • Makala itumie mtindo wa hati za Times New Roman zenye ukubwa wa nukta 12, nafasi baina ya mistari iwe 1.5.
  • Vichwa vya habari katika matini viandikwe kwa muwala kwa kuzingatia viwango (Angalia Mfano, Kichwa cha habari kikubwa, 1.1 Kichwa cha habari kiwango cha pili, na 1.1.1 Kichwa cha habari kiwango cha tatu.
  • Makala itumie mtindo wa APA toleo la 7

 Utumaji wa Makala (Submission)

Orodha Hakiki  Kabla ya kuwasilisha Mswada ( Checklist before Submission)

  • Jina/majina kamili ya waandishi yaandikwe kwa kuanza na jina la kwanza, la kati na la mwisho.
  • Iwapo mwandishi ni zaidi ya mmoja, waandikwe kwa kuanza na mwandishi wa kwanza pamoja na barua pepe zao.
  • Waandishi wote waliotajwa katika msawada kuwa waandishi lazima wakubali kutambulika kama waandishi katika makala.
  • Makala yenye zaidi ya mwandishi mmoja, aainishwe mwandishi wa mawasiliano.
  • Hakikisha jedwali na vielelezo vyote vimepangwa na kupewa nambari na majina.
  • Ikiwa mwandishi ametumia picha au vielelezo vyovyote vinavyohitaji ruhusa kwa wahusika mwandishi anawajibika kuomba ruhusa ya kutumia vielelezo hivyo kabla ya kuwasilisha mswada.

 

Sera ya Faragha (Privacy Statement)

Taarifa binafsi za majina na anwani za barua pepe zinazowekwa kwenye tovuti ya jarida hili zitatumika kwa madhumuni rasmi tu yaliyotajwa na jarida na hazitatumika kwa matumizi mengine yoyote, wala kwa mtu au taasisi nyingine.

MWONGOZO KWA WAANDISHI MAKALA

Waandishi wa makala watakaotuma makala zao kwa ya kuchapishwa katika Jarida la Bahari ya lugha watapaswa kufuata mwongozo ufuatao:

  1. Urefu wa makala usipungue maneno elfu 3000 na usizidi maneno 6500.
  2. Nafasi baina ya mstari ni 1.5
  3. Makala ichapwe kwa hati za Times New Roman ukubwa wa maandishi uwe 12.
  1. Namba za Tiniwayo (footnotes) ziandikwe kwa usahihi na ziwiyane na zilizomo katika makala.
  2. Tiniwayo (footnotes) zisiwe nyingi.
  3. Lugha iwe rasmi na fasaha
  4. Urejeleaji uwe wa mtindo wa APA Toleo la 7.
  5. Makala ifenyiwe uhariri vizuri kabla ya kuwasilishwa; makala ambayo haitapitiwa vyema haitashughulikiwa.
  6. Vichwa vidogo vya habari vipewe nambari kwa kufuata mpangilio wa uandishi wa tasnifu.
  7. Ikisiri isizidi maneno 300
  8. Ukurasa wa kwanza uwe na jina au majina ya waandishi, taasisi wanazotoka na anuwani ya paruapepe.